Saturday, March 31, 2012

Hekima ni nini

Ndugu Zangu,
MFALME Suleiman aliambiwa ndotoni aombe kitu chochote kwa Mungu wake, naye akatii akaomba; “ Ewe Mungu wangu, nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili ili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya, maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi?”

Hivyo basi, Mfalme Suleiman alichagua hekima. Maana, ni Mfalme Suleiman huyo anayekaririwa na vitabu vya dini akitamka, kuwa; “ Watu wangu wanaangamia kwa kukosa hekima”.

Naam, hekima ndilo jambo lililo bora kabisa kwa mwanadamu kuwa nalo. Mwanadamu aliyepungukiwa hekima ana hasara kubwa maishani. Hekima ni tunu na kipaji ambacho Mungu amewajalia watu wake, ili nao waweze kupambanua na kuamua kati ya yaliyo mema na maovu.
mara nyingi nimekuwa nikitafakari mambo ambayo nimekuwa nikijuhusisha kufanya tangu mwaka 2004 nilipohitimu masomo ya sekondari nimeona kuwa kwamba mambo mengi nimekuwa nikiyafanya si kwa sababu nimesoma sana lakini ni kwa hekima/tunu ya Mungu iliyomo ndani yangu. Make kuna vitu nimekuwa nikijihusisha kufanya na kuonekana kuwa bora na wakati mwingine watu kuniuliza kuwa mambo haya nimejifunzia wapi wakati sijawahi kuingia shule ya fani hizo. Ukweli ni kwamba hekima ya Mungu inapita hekima zote. Suleimani aliona kuwa kitu pekee cha kumsaidia katika uongozi wake ni Hekima nami baada ya kukaa na kusoma historia ya mfalme Suleiman nimesikia kuwa na blog hii ya hekima.

Duniani hakuna shule ya hekima. Kuwa na hekima ni kuwa na tunu, kuwa na kipaji ambacho binadamu hujaliwa nacho. Na mwingine atajiuliza; hekima ni nini? Ni ule uwezo wa mwanadamu kuwa na maarifa ya kufahamu kipi cha kufanya, kwanini afanye, wapi na kwa wakati gani. Hivyo basi, hekima ni maarifa, tunaangamia kwa kukosa maarifa, kukosa hekima. Nashauri katika mambo yako yote unayofanya tafuta kuwa na hekima ambayo ilimsaidia mfalme Suleiman kuwaongoza watu wa Mungu lakini pia hekima hii ilimsaidia kuwaongoa wana Israel Kutoka Misri kwenda kanani.

4 comments:

  1. Nakubaliana na mtazamo wako kuhus umuhimu wa hekima na haswa hekima ya Mungu ambayo tunaiita hekima itokayo juu Yak 3:17. Lkn pia kuna hekima ya duniani ambayo unaweza kuiona katika Yak 3:15 sifa za hekima hizi mbili na tofauti zake zimeonyeshwa. biblia imeleeleza kwa krefu sana kuhusu hekima.

    hata hivyo nataka kukushauri usome tena kwa makini kitabu cha wafalme na kutoka kwamba Suleiman hakuhusika katika mchakato wa kuwaongoza wana wa Israel kutoka Misri lkn tunajua kuwa Musa, haruni na Yoshua walikuwa wote na hekima.

    ReplyDelete
  2. Asante wakumbushaji wetu, nanyi Mungu atawalipeni kadri mnavyojitolea kuelimisha umma wake. Amani, busara, hekima na upendo viwe nanyi

    ReplyDelete
  3. Kwa hiyo suleman akuhusika na swala LA ukombozi wa israel au iko vipi ndungu zangu

    ReplyDelete