Tuesday, February 12, 2013

NI NYAKATI ZA MWISHO SASA

Ukiona mambo yanayotokea sasa katika ulimwengu tulionao ni dhahiri kuwa sasa ulimwengu umefika mwisho. Nimeamua kuandika makala hii kwenye blog hii ya hekima baada ya kuchunguza mambo yanayotokea siku kwa siku. Sina malengo ya kufanya uchochezi wa aina yoyote lakini nisikia kusukumwa kusema haya machache ambayo nitayaandika hapa kwa ushirika wa roho wa Mungu.

Ndugu zangu mara nyingi tumekuwa tukishirikiana kwa mambo mengi bila kujari dini wala kabila zetu, lakini tulipofika sasa watu wengi wanatamani kutetea kabila zao na dini pia. Jambo la kujiuliza dini hizi tunazopingania zitatufikisha wapi?

Je dini hizi zimeanzishwa na nani?

Je si wanadamu tu walioanzisha dini hizi, lakini nini faida ya kuua mwanadamu mwenzako?

Ninavyofahamu dini hizi zilizopo zimeanzishwa na wanadamu tu. Na inawezekana kabisa watu hawa walioanzaisha dini wasifike Mbinguni kwani sasa wameshaacha kuzifuata njia ya kweli.

Hakuna haja ya kupigana wakati tunajua kabisa dini zetu ni za kweli na tunaifuata ile kweli ambayo tuliipokea kwa yule aliye tuita na hata akaamua kutoa sadaka kwa ajili yetu.
Lakini pia kitu cha kujiuliza nani ataenda uzimani na dini yake?

Mara zote Mungu huangalia watu wanao mtafuta kwa bidii, na hao ndio Mungu anawaheshimu wala si watu washindanao katika mambo ya dunia hii "Nawapenda wale wanipendao na wanitafutao kwa bidii" Mith 8:17.

Shida tulionayo sasa watu wengi katika ulimwengu huu wanatafuta kuonekana kuwa wao ni bora zaidi kuliko wengine. Na wanapenda kuonyesha ubabe katika taifa hili, si Tanzania tu bali hili ni anguko la Ulimwengu hata ukiangalia kwenye nchi zingunezo.

Lakini nipende kuwakumbusha kuwa vita ya Mtu anayejua kuwa yu sahihi iko katika ulimwengu wa roho wala si katika kumwaga damu ya watu ama wanyama



"Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho (Efe 6:12)."

Kwa nini tuchinjane kwa sababu zisizokuwa za lazima?

Kila mtu atubu aache dhambi zake maana sasa tu katika nyakati za mwisho maana yaliyotabiliwa katika kitabu cha ufunuo wa yohana ndiyo haya yanayofanyika sasa. Ni vema kugeuka tukamrudia Mungu wetu maana yeye ni mwingi wa rehema ataturehema.
Mungu akubariki kwa haya. 
Amen